Mwanzo / GPS Tracking
Kwa Wenye Magari

GPS Tracking ya Magari Tanzania

Fuatilia magari yako moja kwa moja kwa simu na kompyuta, fuatilia mafuta na upate ripoti kulingana na mahitaji yako. Kifaa cha GPS kinaanzia TZS 110,000 na subscription kuanzia TZS 35,000 kwa mwezi.

Unachopata

Unachopata na GPS tracking

Mahali pa gari moja kwa moja

Ona magari yako kwenye simu na kompyuta, historia ya safari na ripoti kulingana na mahitaji yako.

Sensor ya mafuta

Fuatilia kiwango cha mafuta, kujaza mafuta na dalili za upotevu wa mafuta.

Muunganisho na mfumo wako

Tunaweza kuunganisha taarifa za GPS na mfumo wako wa biashara, bei kulingana na mahitaji.

Bei

Bei ya GPS na sensor kwa kila gari

Huduma Bei (TZS) Maelezo
Kifaa cha GPS (tracking device) Kuanzia TZS 110,000 Mara moja kwa kila gari. Bei inategemea aina ya kifaa.
Sensor ya mafuta TZS 270,000 Mara moja, si lazima.
Ufungaji (installation) TZS 50,000 Kwa kila kifaa cha GPS. Ukifungiwa GPS na sensor ya mafuta kwa pamoja: TZS 100,000.
Subscription, magari ndani ya Tanzania TZS 35,000 / mwezi Malipo kuanzia miezi 6.
Subscription, magari yanayotoka nje ya Tanzania TZS 65,000 / mwezi Malipo kuanzia miezi 6.

Mfano: gari moja ndani ya Tanzania lenye GPS (kuanzia 110,000), sensor ya mafuta (270,000), ufungaji (100,000) na subscription ya miezi 6 (6 x 35,000 = 210,000) linaanzia TZS 690,000. Gari linalovuka mpaka linaanzia TZS 870,000.

Maswali

Maswali ya mara kwa mara

Bei ya GPS tracking ya gari ni ngapi?

Kifaa kinaanzia TZS 110,000, ufungaji TZS 50,000 (TZS 100,000 ukifungiwa GPS na sensor ya mafuta), sensor ya mafuta TZS 270,000. Subscription ni TZS 35,000 kwa mwezi ndani ya Tanzania na TZS 65,000 kwa mwezi kwa magari yanayotoka nje ya nchi, malipo kuanzia miezi 6.

Naweza kuona magari kwenye simu?

Ndiyo. Unaweza kufikia mfumo kwa simu na kompyuta, na ripoti hutengenezwa kulingana na mahitaji yako.

Naweza kulipa kwa njia gani?

Tunapokea bank transfer, M-Pesa na mobile money nyingine, na cash.

Pata quotation ya maandishi

Tuambie mahitaji yako. Tunajibu ndani ya saa 2 za kazi. Malipo kwa bank transfer, M-Pesa au cash, kwa awamu ukipenda.

Omba Quotation WhatsApp